MPANGO WA KUTOA MATUZO WA IDARA YA VITA YA USAFRICOM
Wasilisha taarifa kisiri. Tuzwa. Dumisha usalama katika jamii yako.
Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita ya USAFRICOM (DoWRP) ni mpango salama na wenye mafanikio ambao huwatuza watu binafsi kwa kutoa taarifa muhimu na zinazoweza kuthibitishwa zinazodumisha usalama na utulivu wa bara la Afrika, na vikosi vya Marekani na washirika wake barani Afrika.
Mpango wa Kutoa Matuzo wa USAFRICOM DoWRP
Ikiwa una taarifa ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa jeshi la Marekani, toa taarifa za kutahadharisha na unaweza kutuzwa. Taarifa zote, ikijumuisha maelezo kuhusu mtu binafsi, huhifadhiwa kwa njia ya siri na zitaithinishwa na kuthibitishwa kabla ya kutoa tuzo.
Toa Taarifa za Kutahadharisha
Mchakato wa Kutoa Taarifa za Kutahadharisha
USAFRICOM DoWRP inatoa zawadi za fedha au zawadi za aina nyingine kwa watu binafsi wanaotoa taarifa muhimu kuhusu ugaidi na mashambulizi yaliyopangwa dhidi ya vikosi vya Marekani na washirika wake barani Afrika. Utambulisho wa anayetoa taarifa za kutahadharisha hufichwa kabisa. Kadiri taarifa zinavyokuwa za kipekee na muhimu zaidi, ndivyo thamani ya tuzo inayoweza kutolewa inavyoongezeka. Kutathmini thamani ya tuzo kunategemea mambo mengi mbalimbali ambayo yatazingatiwa na maafisa wa USAFRICOM wakati wa mchakato wa uidhinishaji wa tuzo.
- 1 Watu binafsi wanaweza kuwasilisha taarifa kwa njia ya siri kupitia fomu ya kutahadharisha au kupitia nambari ya simu ya eneo uliko.
- 2 Baada ya taarifa za kutahadharisha kupokelewa, taarifa hiyo hutafsiriwa na kushirikiwa na USAFRICOM ili kufanyiwa uchunguzi. Kutokana na wingi wa taarifa za kutahadharisha zinazopokelewa na USAFRICOM, inaweza kuchukua muda kabla ya kushughulikia taarifa zako za kutahadharisha. Tafadhali, kuwa na hakikisho kuwa taarifa zako za kutahadharisha zitapitiwa kwa wakati unaofaa.
- 3 Ikiwa taarifa hizo zitathibitishwa na kuwa na manufaa, USAFRICOM itawasiliana na aliyezitoa, na anaweza kutuzwa hadi dola za Marekani (USD) 5,000,000.
Toa taarifa za kutahadharisha kwa njia salama kwa USAFRICOM
Ili kutoa taarifa za kutahadharisha, tumia fomu ya kutoa taarifa za kutahadharisha kupitia tovuti. Toa maelezo mengi iwezekanavyo, ikijumuisha taarifa zinazowezesha kutambua eneo au anwani zozote zinazohusiana na taarifa za kutahadharisha, na nambari ya simu au baruapepe ambayo tunaweza tumia kukufikia.
Taarifa zote zinazotolewa, ikijumuisha maelezo kuhusu mtu binafsi, zitahifadhiwa kwa njia ya siri.
Unaweza pia kubofya kitufe kilicho hapa chini ili kuthibitisha kama USAFRICOM ina nambari ya simu ya ndani katika nchi yako. Ikiwa ipo, unaweza kutoa taarifa kwa kuipiga.
Je, Mpango Huu Hutuza Taarifa za Aina Gani?
USAFRICOM DoWRP inatuza watu binafsi fedha kwa kutoa taarifa muhimu kuhusu ugaidi na mashambulizi yaliyopangwa dhidi ya vikosi vya Marekani na washirika wake barani Afrika. Utambulisho wa mtoaji wa taarifa za kutahadharisha hufichwa kabisa. Je, una taarifa zozote kuhusu mada hizi? Tafadhali toa taarifa za kutahadharisha hata kama unafikiri maelezo yako si muhimu. Huwa kuna uchunguzi mwingi ambao hutokea kwa wakati mmoja. Kwa hivyo taarifa zako za kutahadharisha zinaweza kusaidia na unaweza kutuzwa.
Maombi ya Dharura ya Habari Zinazohitajika
USAFRICOM DoWRP kwa sasa inatafuta taarifa za kutahadharisha kuhusu visa vifuatavyo vilivyotokea moja kwa moja. Tunaendelea kukaribisha taarifa kuhusu ugaidi na mashambulizi yaliyopangwa dhidi ya vikosi vya Marekani na washirika wake, mbali na visa vilivyotokea moja kwa moja.
Mpango wa Matuzo wa DoW unatoa zawadi ya kifedha kwa taarifa zitakazosaidia kupata wanajeshi wawili wa Jeshi la Wanamaji la Marekani (U.S. Navy SEALs) ambao walitoweka katika Ghuba ya Aden tarehe 11 Januari mwaka wa 2024.
Pakia ZaidiMaswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu USAFRICOM DoWRP.
Je, Idara ya Vita ina mamlaka gani kufanya DoWRP?
Mamlaka ya kuendesha DoWRP ni Sheria ya Marekani, Toleo la mwaka wa 2012, Nyongeza ya 4, Anwani ya 10 – vVIKOSI VYA WANAJESHI, Anwani Ndogo ya A – Sheria ya Jumla ya Wanajeshi, SEHEMU YA 1 – MFUMO WA UONGOZI NA MAMLAKA YA JUMLA YA WANAJESHI, SURA YA 3 – MAMLAKA NA KAZI KWA UJUMLA, Kifungu cha 127b - Mpango wa Matuzo wa Idara ya Vita.
Je, kiasi cha malipo ya tuzo huamuliwa vipi?
USAFRICOM DoWRP hutoa matuzo ya pesa, au matuzo ya aina nyingine. Kiasi hutofautiana kutegemea na ubora wa taarifa zilizotolewa, umuhimu wake kwa shughuli za vikosi vya Marekani na za washirika wake, na kiwango cha tishio lililozuiwa au kuepukika. Kadiri maelezo yanavyozidi kuwa ya kipekee na muhimu, ndivyo thamani ya tuzo inavyoongezeka.
Je, malipo ya tuzo hutolewaje?
Baada ya taarifa za kutahadharisha zilizotolewa kufanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa kuwa muhimu na za kweli, afisa wa USAFRICOM DoWRP atawasiliana na aliyezitoa kwa njia ya tahadhari na kumtuza ipasavyo kupitia zawadi ya pesa au zawadi nyingineyo. Zawadi nyingi hulipwa kwa njia ya pesa taslimu.
Je, mpango huu utatafuta habari ya aina gani? Ni habari gani zitatuzwa?
USAFRICOM DoWRP inatuza kwa kutoa taarifa na usaidizi usio na madhara ambao huwezesha vikosi vya Marekani na washirika wake kupambana na ugaidi pamoja na kulinda vikosi vya Marekani na washirika wake dhidi ya mashambulizi yaliyopangwa. Mfano unaweza kuwa kuionya Serikali ya Marekani kuhusu tishio lililopangwa dhidi ya vikosi vya Marekani au washirika wake au kuripoti kuhusu watubinafsi waliohusika na mashambulizi ya awali au yaliyopangwa dhidi ya vikosi vya Marekani na washirika wake.
USAFRICOM DoWRP ni nini na hufanya nini?
USAFRICOM DoWRP ilianzishwa ili kuwatuza watu wanaofaa kutuzwa wanaotoa taarifa au usaidizi usio na madhara ambao huwezesha vikosi vya Marekani na washirika wake kupambana na ugaidi na kulinda vikosi vya Marekani na washirika wake.
Nitajuaje kuwa taarifa niliotoa ni salama?
Usalama na usiri ni vipengele muhimu vya USAFRICOM DoWRP. Taarifa zote zinatolewa kwa mpango huu hupewa husimbwa na kutumiwa kwa njia salama. Utambulisho wa wanaotoa taarifa za kutahadharisha hufichwa kabisa. Jifahamishe zaidi.
USAFRICOM ni nani?
Komando ya Marekani na Afrika (USAFRICOM) ni komando ya pamoja ra kupigana ya Idara ya Vita ya Marekani ilio na wajibu wa kusimamia operesheni za kijeshi za Marekani barani Afrika. Pamoja na washirika na wabia wake, USAFRICOM hutekeleza wajibu muhimu wa kudumisha usalama na utulivu wa kikanda.