Usalama wa Taarifa
Usalama na usiri ni vipengele muhimu vya Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita wa USCENTCOM. Taarifa zote zinazowasilishwa kwa mpango huu zimesimbwa na kutumiwa kwa njia salama. Utambulisho wa anayetoa taarifa za kutahadharisha hufichwa kabisa.
Jinsi Tunavyoweka Taarifa Zako kwa Njia Salama
- Tunachukulia usalama wa taarifa kukuhusu wewe binafsi kwa uzito na tumeweka ulinzi thabiti wa kiufundi na wa shirika.
- Ingawa hakuna mfumo unaoweza kuhakikishwa kuwa salama kwa asilimia 100, tunaendelea kufanya kazi pasipo na kusita ili kuimarisha ulinzi wetu.
- Katika tukio ambalo halitarajiwi kutokea ambapo mtu atajaribu kukwepa usalama wetu, tafadhali fahamu kwamba tumejitolea kushughulikia hali haraka na kwa ufanisi.Hata hivyo, kama ilivyo na shughuli yoyote mtandaoni, kushiriki taarifa mtandaoni huwan a hatari fulani.
- Ili kusaidia kuweka data yako salama, tunapendekeza utembelee tovuti yetu kwa kutumia mtandao salama.
Ni Taarifa Gani Tunazokusanya Kiotomatiki
Unapotembelea tovuti yetu, tunakusanya data kiotomatiki kama vile anwani yako ya IP, aina ya kivinjari, maelezo ya kifaa unachotumia, mfumo wa uendeshaji, eneo kwa ujumla na ruwaza ya matumizi ya tovuti. Pia huwa tunakusanya ripoti za hitilafu ikiwa mfumo utakumbana na matatizo. Data hii hukusanywa kupitia vidakuzi na teknolojia sawia.
Jinsi Tunavyotumia Taarifa
- Kulinda Huduma zetu. Tunaweza kutumia taarifa zako kama sehemu ya juhudi zetu za kufanya Tovuti yetu kuwa salama (kwa mfano, kwa kufuatilia na kuzuia ulaghai.)
- Kutekeleza sheria, masharti, na sera zetu zirandane na mahitaji ya kisheria na utekelezaji wa sheria.
- Kukamilisha na kuwezesha shughuli inayoendelea.
- Kusimamia na kuendesha Tovuti na mfumo wake.
- Kufanya utafiti na maendeleo.
- Kutekeleza mambo yalioidhinishwa kisheria.
Je, Unataka Taarifa Zaidi?
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia data, tunakuhimiza kutembelea Sera kamili ya Faragha ya Idara ya Vita ya Marekani hapa.