Notisi kuhusu faragha

Asante kwa kuchagua kuwa sehemu ya jamii yetu kupitia Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita. Tumejitolea kulinda taarifa kukuhusu wewe binafsi na haki yako ya kuwa na faragha.

Notisi hii ya faragha inaeleza jinsi tunavyoweza kutumia taarifa yako ikiwa:

  • Utatembelea tovuti yetu kupitia https://dowrewardsprogram.net.
  • Utajumuika nasi kupitia njia zingine zinazohusiana – ikijumuisha matangazo ya biashara au hafla.

Katika notisi hii ya faragha, tukirejelea:

  • ”Tovuti,” tunarejelea tovuti yetu yoyote ambayo inarejelea au ina kiungo cha kukupeleka kwa sera hii.
  • ”Huduma,” tunarejelea tovuti yetu, na huduma zingine zinazohusiana, ikijumuisha matangazo ya biashara au hafla.

Madhumuni ya notisi hii ya faragha ni kukuelezea kwa njia iliyo wazi zaidi kuhusu ni taarifa gani tunazokusanya, jinsi tunavyozitumia na una haki gani kuhusiana nazo. Ikiwa kuna masharti yoyote katika notisi hii ya faragha ambayo hukubaliani nayo, tafadhali acha kutumia huduma zetu mara moja.

Tafadhali soma notisi hii ya faragha kwa makini, kwa sababu itakusaidia kuelewa tunachofanyia taarifa tunazokusanya.

Taarifa Zinazokusanywa Kiotomatiki

Kwa Ufupi: Baadhi ya taarifa – kama vile anwani yako ya Protokali ya Intaneti (IP) na/au sifa za kivinjari na kifaa unachotumia – hukusanywa kiotomatiki unapotembelea Tovuti yetu.

Tunakusanya taarifa fulani kiotomatiki unapotembelea, kutumia, au kupitia Tovuti yetu. Maelezo haya hayaonyeshi utambulisho wako mahususi (kama vile jina lako au maelezo ya jinsi ya kuwasiliana nawe), lakini yanaweza kujumuisha maelezo ya kifaa na matumizi yake, kama vile anwani yako ya IP, kivinjari na sifa za kifaa unachotumia, mfumo wa uendeshaji, lugha unayopendelea, URLs ulizotumia, nchi, eneo, maelezo kuhusu jinsi na wakati unapotumia Tovuti yetu na taarifa nyingine za kiufundi. Taarifa hizi zinahitajika kimsingi ili kudumisha usalama na uendeshaji wa Tovuti yetu, na kwa ajili ya uchanganuzi wa ndani na kwa madhumuni ya kutoa ripoti.

Kama mashirika mengi ya biashara, sisi pia hukusanya taarifa kupitia vidakuzi na teknolojia sawia.

Taarifa tunazokusanya

Taarifa tunazokusanya ni pamoja na:

  • Data ya Kumbukumbu na Matumizi: Data ya kumbukumbu na matumizi inahusiana na huduma, uchunguzi, matumizi na maelezo ya utendakazi ambayo huduma zetu hukusanya kiotomatiki unapotembelea au kutumia Tovuti yetu na ambayo huwa tunarekodi katika faili za kumbukumbu. Kutegemea na jinsi unavyojumuika nasi, data hii ya kumbukumbu inaweza kujumuisha anwani yako ya IP, maelezo kuhusu kifaa unachotumia, aina ya kivinjari na mipangilio yake na maelezo kuhusu shughuli zako kwenye Tovuti (kama vile tarehe/saa inayohusishwa na matumizi yako, kurasa na faili ulizotazama, utafutaji na hatua nyingine unazochukua, kama vile vipengele unavyotumia), maelezo kuhusu kifaa wakati unapokitumia (kama vile shughuli za mfumo, ripoti za hitilafu (wakati mwingine hurejelewa kama ‘data wakati kifaa kinapoacha kufanya kazi’) na mipangilio ya maunzi).

  • Data kuhusu Kifaa: Huwa tunakusanya data kuhusu kifaa kinachotumika kama vile maelezo kuhusu kompyuta yako, simu yako, kipakatalishi chako au kifaa kingine unachotumia kutembelea Tovuti. Kutegemea na kifaa kinachotumiwa, data kuhusu kifaa hiki inaweza kujumuisha taarifa, kama vile kifaa cha anwani yako ya IP (au seva mbadala) na nambari za utambulisho wa programu unayotumia, eneo, aina ya kivinjari, muundo wa maunzi, mtoa huduma za Intaneti, na/au mtoa huduma za simu, mfumo wa uendeshaji na maelezo kuhusu usanidi wa mfumo.

  • Data kuhusu Eneo: Tunakusanya data kuhusu eneo, kama vile taarifa kuhusu eneo la kifaa chako, ambazo zinaweza kuwa sahihi au zisizo sahihi. Kiasi cha taarifa tunazokusanya hutegemea aina na mipangilio ya kifaa unachotumia kutembelea Tovuti. Kwa mfano, tunaweza kukusanya data ya eneo la kijiografia inayotufahamisha kuhusu eneo uliko (kwa kuzingatia anwani yako ya IP). Unaweza kuchagua kutoturuhusu kukusanya taarifa hizi kwa kukataa ufikiaji wa taarifa hizi au kwa kuzima mipangilio yako ya Eneo kwenye kifaa chako. Hata hivyo kumbuka, ukichagua kujiondoa, huenda usiweze kutumia vipengele fulani vya Huduma zetu.

Je, Huwa Tunatumiaje Taarifa Zako?

Tunatumia taarifa zinazokusanywa kuhusu watu binafsi kupitia Tovuti yetu kwa madhumuni mbalimbali ya biashara yaliyofafanuliwa hapo chini.

Tunaweza kutumia data yako kwa madhumuni yafuatayo:

  • Kulinda Huduma zetu. Tunaweza kutumia taarifa kukuhusu kama sehemu ya juhudi zetu za kufanya Tovuti yetu kuwa salama (kwa mfano, kwa kufuatilia na kuzuia ulaghai).
  • Kutekeleza sheria, masharti, na sera zetu zirandane na mahitaji ya kisheria na utekelezaji wa sheria.
  • Kukamilisha na kuwezesha shughuli inayoendelea.
  • Kusimamia na kudumisha Tovuti na mfumo wake.
  • Kufanya utafiti na maendeleo.
  • Kutekeleza mambo yalioidhinishwa kisheria.

Je, Tunatumia Vidakuzi na Teknolojia Nyingine za Kufuatilia?

Kwa Ufupi: Tunalenga kulinda taarifa kukuhusu wewe binafsi kupitia mfumo wa shirika na hatua za kiufundi za usalama.

Tumetekeleza hatua mwafaka za usalama za kiufundi na za shirika zilizoundwa ili kulinda usalama wa taarifa zozote kuhusu mtu binafsi tunazoshughulikia. Hata hivyo, licha ya ulinzi na jitihada zetu za kulinda taarifa zako, hakuna utumaji wa kielektroniki mtandaoni au teknolojia ya kuhifadhi taarifa inayoweza kudhibitishwa kuwa salama kwa asilimia 100, kwa hivyo hatuwezi kuahidi au kuhakikisha kwamba wadukuzi, wahalifu wa mtandaoni, au wahusika wengine ambao hawajaidhinishwa hawataweza kupiku usalama wetu, na kukusanya, kufikia, kuiba, au kurekebisha taarifa zako isivyofaa. Ingawa tutafanya yote tunayoweza kufanya, taarifa kukuhusu wewe binafsi, utumaji wa taarifa kukuhusu kwenda na kutoka kwa Tovuti yetu ina hatari kwako mwenyewe. Unapaswa kutembelea Tovuti tu katika mazingira salama.

Vidhibiti vya Vipengele vya Kufanya Usifuatiliwe

Vivinjari vingi vya wavuti na baadhi ya mifumo ya uendeshaji ya simu na programu za simu hujumuisha kipengele cha Kufanya Usifuatiliwe (“DNT”) au mpangilio unayoweza kuwasha ili kuashiria unapendelea faragha ili data kuhusu shughuli zako za kuvinjari mtandaoni zisifuatiliwe wala kukusanywa. Kwa sasa, hakuna kiwango sare cha teknolojia cha kutambua na kutekeleza vidokezo vya DNT kimekamilika. Kwa hivyo, kwa sasa hatushughulikii vidokezo vya kivinjari cha DNT au mfumo mwingine wowote unaowasilisha kiotomatiki chaguo lako la kutotaka kufuatiliwa mtandaoni. Ikiwa kiwango cha ufuatiliaji mtandaoni kitapitishwa ambacho ni lazima tufuate katika siku zijazo, tutakujulisha kuhusu utaratibu huo katika toleo lililosahihishwa la notisi hii ya faragha.

Notisi kwa Watu Wanaotembelea Tovuti hii Nje ya Marekani

Huduma zetu zinadhibitiwa na kuendeshwa nasi kutoka Marekani, hutolewa kwa wakazi wa Marekani, na hazikusudiwi kutuweka chini ya sheria au mamlaka ya jimbo, nchi, au eneo lolote isipokuwa tu zile za Marekani. Taarifa zozote utakazotoa kupitia matumizi ya Huduma hii zinaweza kuhifadhiwa na kutumiwa, kuhamishwa kati ya nchi na kufikiwa kutoka Marekani na nchi nyingine ambazo haziwezi kukuhakikishia kiwango sawa cha ulinzi wa taarifa kuhusu mtu binafsi kama cha nchi unamoishi. Ikiwa hutaki maelezo kukuhusu yaondoke katika nchi yako, tafadhali usitoe taarifa kama hizo kwa Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita na wala usitumie tovuti yetu. Kwa kutoa taarifa kukuhusu kwa Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita, unakubali waziwazi uhamishaji wa taarifa zako hadi Marekani.

Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita au watoa huduma wake wanaweza pia kuhamisha taarifa kukuhusu kutoka Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA) hadi nchi nyingine, ambazo baadhi yake bado hazijabainishwa na Tume ya Ulaya ili kutoa kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kulingana na viwango vya EEA. Kwa uhamishaji hadi kwa nchi zisizohitaji kiwango cha ulinzi wa data ambacho kinakidhi viwango vya EEA, Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita hutumia mbinu mbalimbali za kisheria kulinda taarifa kukuhusu, ikiwa ni pamoja na masharti ya kimkataba na uhakikisho kupitia maandishi kutoka kwa watoa huduma.

Tutashughulikia taarifa kukuhusu kwa kuzingatia Sera hii ya Faragha bila kujali maelezo kukuhusu wewe binafsi yamehifadhiwa au kufikiwa kutoka wapi.

Viungo hadi kwa Tovuti za Nje

Viungo hadi kwa tovuti zilizo nje ya Serikali ya Shirikisho ya Marekani au matumizi ya majina ya biashara, kampuni au mashirika ndani ya tovuti ya Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita ni kwa manufaa ya mtumiaji. Matumizi kama hayo hayajumuishi uidhinishaji rasmi au uidhinishaji wa Mpango wa Kutoa Matuzo wa Idara ya Vita wa Marekani wa tovuti, bidhaa au huduma yoyote ya sekta ya kibinafsi.

Sheria ya Ulaghai na Matumizi Mabaya ya Kompyuta

Majaribio yasiyofaa ya kupakia taarifa na/au kubadilisha taarifa katika tovuti hii hayaruhusiwi kamwe na yanaweza kufunguliwa mashtaka chini ya Sheria ya Ulaghai na Matumizi Mabaya ya Kompyuta ya mwaka wa 1986, 18 U.S.C. § 1030, na kifungu cha 1001 cha Anwani ya 18.

Sera ya Faragha ya Idara ya Vita

Unaweza kutazama sera ya faragha ya tovuti ya Idara ya Vita ya Marekani kupitia:

https://www.defense.gov/Legal-Administrative/Privacy-Security/

Jinsi ya Kuwasiliana Nasi

Tunakaribisha maoni ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera yetu ya faragha au matumizi ya taarifa ulizotoa. Iwapo ungependa kupata taarifa zaidi kuhusu Mpango wa Faragha wa Idara ya Vita ya Marekani, tafadhali tembelea Faragha (defense.gov).